ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

WALIMU WAKUU 50 KUTOKA WILAYA ZA NACHINGWEA, MTAMA, LINDI NA RUANGWA WAENDELEA NA MASOMO YA UONGOZI ADEM

22 Aug, 2022
WALIMU WAKUU 50 KUTOKA WILAYA ZA NACHINGWEA, MTAMA, LINDI NA RUANGWA WAENDELEA NA MASOMO YA UONGOZI ADEM

Walimu Wakuu na Walimu Wakuu wasaidizi 50 kutoka Wilaya za Nachingwea, Lindi, Ruangwa na Mtama waliopata ufadhili wa kusoma Stashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (DEMA) inayoendeshwa ADEM Bagamoyo wamekamilisha awamu ya pili ya masomo yao ambapo walifika Bagamoyo na kuanza masomo yao tarehe 1 Agosti, 2022 na wamehitimisha awamu hiyo tarehe 20 Agosti, 2022. Awamu ya tatu ya mafunzo hayo itaendelea Mwezi Oktoba, 2022 ambapo watafika tena ADEM Bagamoyo kuendelea na masomo yao katika awamu hiyo.Katika awamu ya kwanza Walimu hao 50 walifika kwa mara kwanza kuanza masomo yao ya Ungozi na Usimamizi wa Elimu kwa ngazi ya Stashahada mnamo Mwezi Machi 2022

Programu hiyo inaendeshwa na ADEM kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU) kwa kipindi cha miaka miwili ili kuwajengea uwezo walimu hao katika masuala ya Uongozi na Usimamizi fanisi wa Shule wanazosimamia na kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji wa Wilaya hizo, ambapo watakapohitimu masomo yao watatunukiwa Stashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (DEMA).