ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

JISAJILI SASA KWA AJILI YA MAFUNZO YA UONGOZI NA USIMAMIZI FANISI WA SHULE KWA MAMENEJA NA WALIMU WAKUU WA MKOA WA ARUSHA, DODOMA NA DAR ES SALAAM

13 Jan, 2025

Wakala wa maendeleo ya Uongozi wa Elimu utaendesha mafunzo ya uongozi, usimamizi na utawala wa elimu kwa walimu wakuu na mameneja wa shule za msingi zisizo za Serikali kuanzia tarehe 20 Januari, 2025 hadi tarehe 30 Machi, 2025. Hii ni katika kutekeleza maelekezo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo aliyoyatoa kwa Wakala kuendesha mafunzo hayo hadi kufikia mwezi Machi, 2025. 

Hivyo mafunzo haya yatafanyika kuanzia tarehe 20-30 Machi, 2025 katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na yataanzia katika Mikoa ya Arusha, Dodoma na Dar Es Salaam. Ada ya kushiriki mafunzo haya ni Shilingi 970,000/= kwa Meneja na Mwalimu Mkuu na Shilingi 485,000/= kwa mshiriki mmoja itakayogharamia i) gharama za ufundishaji, ii) Cheti cha Mshiriki wa mafunzo, iii) Chakula - Chai ya asubuhi, Chakula cha mchana na Chai hya jioni, vifaa vya mafunzo pia kitabu kuhusu Uongozi, usimamizi na Utawala Bora wa elimu. Ili kujisajili kwa ajili ya kushiriki mafunzo haya tafadhali fuata maelekezo yafuatayo. Mwisho wa kujisajili ni siku mbili kabla ya mafunzo kufanyika katika Mkoa wako, 2025

BONYEZA LINK HII ILI KUFANYA USAJILI WA MAFUNZO HAYA