PAKUA HAPA FOMU YA KUJIUNGA NA KOZI ZA ADEM KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026 DIRISHA LA MWEZI SEPTEMBA
PAKUA HAPA FOMU YA KUJIUNGA NA KOZI ZA ADEM KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026
Mtendaji Mkuu anawatangazia walimu wote wanaopenda kujiendeleza katika Kozi zinazotolewa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu – ADEM kwa mafunzo ya muda mrefu ya Stashahada (DIPLOMA) kwa mwaka wa masomo 2025/2026 Dirisha la Mwezi Septemba katika Kampasi za Bagamoyo, Mbeya na Mwanza kuwa maombi yameanza kupokelewa kwa Kozi zifuatazo:
Stashahada ya Uongozi, Usimamizi na Utawala wa Elimu (Diploma in Education Leadership, Management and Administration-DELMA) na
Stashahada ya Uthibiti Ubora wa Shule (Diploma in School Quality Assurance-DSQA)
SIFA ZA KUJIUNGA
Mwombaji awe ni Mwalimu ambaye amehitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Daraja la III A; AU Stashahada ya Ualimu inayotambulika na Serikali; AU Shahada ya Ualim; AU Shahada ya Uzamili ya Ualimu;
Mwombaji awe na ufaulu angalau D 4 katika cheti chake cha kidato cha NNE
Maombi yatumwe kwenye anuani ya Barua Pepe iliyopo katika Fomu ya kujiunga
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kwa simu:
Bagamoyo: 0752 839 400, 0786 848 497
Mwanza: 0713 714 616
Mbeya: 0765 518 584