ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

Stashahada ya Uthibiti Ubora wa Shule

MAFUNZO YA STASHAHADA YA UTHIBITI UBORA WA SHULE (DIPLOMA IN SCHOOL QUALITY ASSURANCE) DSQA

ADEM inawatangazia walimu wote wa Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ualimu, Vyuo vya maendeleo ya Wananchi na Vyuo vya ufundi stadi (VET) kuwa maombi yanapokelewa kwa Mwaka wa Masomo 2022/2023.

WALENGWA WA MAFUNZO

1. Walimu waliopo kazini katika ngazi zote za elimu

2. Viongozi wa elimu katika ngazi ya Shule, Kata Halmashauri na Mkoa.

3. Wathibiti Ubora wa Shule

SIFA ZA KUJIUNGA

Mwombaji awe ni mwalimu mwenye uzoefu usiopungua miaka 03 kazini, na ufaulu wa CSEE awe na ufaulu wa masomo manne na angalau C moja katika masomo yasiyo ya dini.

UTARATIBU WA MAOMBI

Muombaji anatakiwa kusoma maelekezo na kujaza fomu inayopatikana katika tovuti ya ADEM: www.adem.ac.tz

MUDA WA MAOMBI

Tarehe 1/04/2022 hadi tarehe 30/09/2022

MUDA WA MAFUNZO

Miaka miwili au mihula minne yenye Wiki 15 kila mmoja. Mafunzo yataanza Mwezi Oktoba 2022.

KAMPASI ZA ADEM

Bagamoyo, Mbeya na Mwanza, mwombaji atachagua kituo anachotaka kusomea.

MAWASILIANO

Tuma barua/fomu yako ya maombi kupitia barua pepe: admission@adem.ac.tz AU MTENDAJI MKUU - ADEM S.L.P 71 BAGAMOYO

Kwa maelezo zaidi Wasiliana nasi kwa Simu Na. 0765140487 (ADEM – Bagamoyo) / 0712690778 (ADEM – Vituo vyote)