Stashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (DEMA)
MAFUNZO YA STASHAHADA YA UONGOZI NA USIMAMIZI WA ELIMU (DIPLOMA IN EDUCATION MANAGEMENT AND ADMINISTRATION) DEMA
ADEM inawatangazia walimu wote wa Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ualimu, Vyuo vya maendeleo ya Wananchi na Vyuo vya ufundi stadi (VET) kuwa maombi yanapokelewa kwa Mwaka wa Masomo 2022/2023.
WALENGWA WA MAFUNZO
1. Walimu waliopo kazini katika ngazi zote za elimu
2. Viongozi wa elimu katika ngazi ya Shule, Kata Halmashauri na Mkoa.
3. Wathibiti Ubora wa Shule
UTARATIBU WA MAOMBI
Mwombaji anatakiwa kusoma maelekezo na kujaza fomu inayopatikana katika tovuti ya ADEM: www.adem.ac.tz
MUDA WA MAOMBI
Tarehe 01/04/2022 hadi tarehe 30/09/2022
SIFA ZA KUJIUNGA
Mwombaji awe ni mwalimu mwenye uzoefu usiopungua miaka 03 kazini, na ufaulu wa CSEE awe na D nnena katika masomo yasiyo ya dini.
MUDA WA MAFUNZO
Miaka miwili au mihula minne yenye Wiki 15 kila mmoja. Mafunzo yataanza Mwezi Oktoba 2022.
KAMPASI ZA ADEM
Bagamoyo, Mbeya na Mwanza, mwombaji atachagua kituo anachotaka kusomea.
MAWASILIANO
Tuma barua/fomu yako ya maombi kupitia barua pepe: admission@adem.ac.tz AU MTENDAJI MKUU - ADEM S.L.P 71 BAGAMOYO
Kwa maelezo zaidi Wasiliana nasi kwa Simu Na. 0679 649443 ADEM - MWANZA 0786 624 512 ADEM - MBEYA 0765 140487 ADEM - Bagamoyo 0712 690778 ADEM - Vituo vyote