ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

ADEM YAENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI NA USIMAMIZI WA SKULI KWA WALIMU WAKUU NA WALIMU WA TAALUMA 96 ZANZIBAR

04 Jul, 2022
ADEM YAENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI NA USIMAMIZI WA SKULI  KWA WALIMU WAKUU NA WALIMU WA TAALUMA 96 ZANZIBAR

Walimu Wakuu na Walimu wa Taaluma wa Skuli za Sekondari wamepatiwa mafunzo na Wataalam wa ADEM juu ya Uongozi na Usimamizi wa Skuli zao. Mafunzo hayo kwa awamu ya kwanza yanaendeshwa kwa Walimu hao wapatao 96 wanaotoka Mkoa wa Kusini Unguja unaojumuisha Walimu kutoka Wilaya ya Kati na Wilaya ya Kusini.
Mtendaji Mkuu ADEM, Dkt Siston Masanja Mgullah amesema Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku tano yakilengankuwajengea uwezo Walimu hao waweze kusimamia Ufundishaji na Ujifunzaji katika Skuli zao, kusimamia nidhamu ya Walimu  na Uwajibikaji, kusimamia mitaala, kufahamu na kusimamia itifaki, kufanya unasihi kwa wanafunzi na wafanyakazi na kuwajenga walimu wapya wanaoanza kazi kiutendaji na kimaadili.
Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa Skuli kwa Walimu Wakuu na Walimu wa Taaluma wa Skuli za Sekondari Mkoa wa Kusini Unguja yamefadhiliwa na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)
Mafunzo haya yanafanyika kwa awamu ambapo katika awamu ya kwanza yamefanyika kwa Walimu Wakuu na Walimu wa Taaluma wa Skuli za Sekondari wa Mkoa wa Kusini Magharibi kuanzia tarehe 13-17 Juni 2022 kisha yataendelea katika Mikoa ya Kaskazini Unguja, Mkoa wa Kati, Kusini Pemba na Kaskazini Pemba.