ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

WAHITIMU 125 WA ADEM WAPATIWA MAFUNZO YA TEHAMA

21 Sep, 2026
WAHITIMU 125 WA ADEM WAPATIWA MAFUNZO YA TEHAMA

Jumla ya wahitimu 125 kutoka Kampasi za ADEM Bagamoyo na Mwanza wamepatiwa mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), yaliyofanyika tarehe 29–30 Agosti 2026, kwa lengo la kuwaongezea ujuzi wa kidijitali utakaowawezesha kuwa na ufanisi katika maeneo ya Kazi

 

Mafunzo hayo yalilenga kuwaandaa wahitimu kutumia teknolojia kwa ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ya kitaaluma na kiutendaji, pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia katika mazingira ya kazi.

 

Mafunzo hayo yalijikita katika maeneo makuu yafuatayo:

 

1. Advanced Office Package

2. Cloud and Digital Collaboration

3. Graphics Design

4. Cybersecurity and Data Protection

5. Digital Communication

6.Artificial Intelligence (AI)

 

Mafunzo hayo yalitolewa kwa njia ya vitendo, huku wahitimu wakipata fursa ya kujifunza na kutumia zana mbalimbali za TEHAMA zinazoweza kuwasaidia kuongeza ufanisi, ubunifu na tija katika utekelezaji wa majukumu yao.

 

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za ADEM kuwaandaa wahitimu wenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na mazingira ya kazi yanayotegemea teknoloji ili wanapokwenda katika maeneo yao ya kazi waweze kutumia TEHAMA kuboresha utendaji na utoaji wa huduma.

 

Mafunzo hayo yamehitimishwa kwa wahitimu kutunukiwa Vyeti vya Ushiriki (Certificate of Attendance) kama uthibitisho wa kushiriki katika mafunzo hayo.