ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

ELIMU JAMII YATOLEWA KWA WANACHUO NA WATUMISHI WA ADEM

16 May, 2025
ELIMU JAMII YATOLEWA KWA WANACHUO NA WATUMISHI WA ADEM

📍Bagamoyo
🗓️15 Mei, 2025

Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Dkt. Alphonce Amuli tarehe 15 Mei, 2025 amewasisitiza Wanachuo kuzingatia maelekezo na Elimu ya kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI, homa ya Ini, kupiga vita rushwa na kuunga mkono Mapambano dhidi ya Rushwa, maelekezo kuhusu namna ya kujikinga, pia kupambana na Majanga hasa ya Moto. 

Dkt. Amuli amezungumza hayo wakati wa zoezi maalumu la utoaji elimu kuhusu masuala ya kijamii yanayogusa kulinda afya ya mwili na afya ya akili, kujihami na majanga pamoja na vita dhidi ya rushwa. Zoezi hilo hufanyika mara moja kila mwaka ili kuwajengea uwezo wanachuo na watumishi katika nyanja hizo ili kuchagiza kujitambua, kulitumikia Taifa kwa uzalendo na kila mmoja kuwajibika kwa afya yake binafsi. 

Wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, TAKUKURU Bagamoyo na Jeshi la Zimamoto Bagamoyo wamewajengea uwezo wanachuo na watumishi katika maeneo husika ambapo pia katika zoezi hilo pia Watumishi na Wanafunzi wamepata fursa ya kujitolea damu kwa hiyari ili kuchangia benki ya damu ya Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.