ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

PAKUA HAPA FOMU YA KUJIUNGA NA KOZI ZA ADEM 2025/2026-MARCH INTAKE

06 Feb, 2025

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM anawatangazia walimu wote wanaotaka kujiendeleza katika Diploma za Uongozi na Usimamizi wa Elimu-DELMA na Diploma ya Uthibiti Ubora wa Shule-DSQA zinazotolewa na ADEM kuwa dirisha la kupokea maombi la Mwezi Machi lipo wazi.

Kozi hizo zinatolewa katika Kampasi ya Bagamoyo, Mbeya na Mwanza katika mfumo wa Residential yaani kuwa chuoni full time na ODL/Blended yaani kusoma kipindi cha likizo wakati shule zinapokuwa zimefungwa.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 02 Machi, 2025 
Karibu ujiunge sasa.
Fomu ya kujiunga inapatikana katika tovuti yetu ya www.adem.ac.tz

Kwa mawasiliano zaidi tafadhali tupigie:
0712711241-Bagamoyo
0752696569-Mwanza
0765518584-Mbeya

PAKUA HAPA FOMU YA KUJIUNGA NA KOZI ZA ADEM DIRISHA LA MWEZI MACHI