ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

WAZIRI MKENDA AZINDUA PROGRAMU YA KUIMARISHA ELIMU YA AWALI NA MSINGI

07 Jun, 2022
WAZIRI MKENDA AZINDUA PROGRAMU YA KUIMARISHA ELIMU YA AWALI NA MSINGI

Na-WyEST-Arusha

Serikali kwa ufadhili wa Benki ya Dunia imezindua program ya kluimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika Shule za awali na msingi -BOOST itakayogharimu shilingi Trilioni 1.15

Akizungumza karika uzinduzi huo uliofanyika Juni 6, 2022 jijini Arusha, Prof Mkenda amesema Programu hiyo itatekelezwa kwa miaka mitano itawezesha kuboresha miundombinu ya Shule za Msingi ambapo madarasa 12000 yatajengwa, uimarishaji wa mpango wa shule salama katika shule 600, kuimarisha uwiano wa uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya awali na kuboresha vifaa na njia za ufundishaji katika madarasa ya elimu ya awali Pamoja na uwekaji wa vifaa vya TEHAMA katika Shule za msingi na vyuo vya walimu.

Waziri Mkenda amewataka watendaji wote katika ngazi ya Wizaran na Taasisi watakaohusika na  utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Programu kufanya kazi kwa bidi na maarifa ili kufikia lengo kila mwaka na kuzingatia vigezo  na viwango vyote vilivyowekwa ili kuondoa changamoto zote ambazo zinaweza kukwamisha program hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Mara Warwick amesema kuwa program ya BOOST itanufaisha wanafunzizaidi ya Milioni 12 katika eneo la Tanzania Bara.

Wakala wa maendeleo ya Uongozi wa Elimu ADEM ni moja kati  ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itakayotekeleza program ya BOOST itakayoendeshwa kwa kipindi cha miaka mitano.