ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

WAWEZESHAJI 255 WATAKAOENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI, USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA SHULE KWA WALIMU WAKUU 4,516 WAPATIWA MAFUNZO

21 Sep, 2023
WAWEZESHAJI 255 WATAKAOENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI, USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA SHULE KWA WALIMU WAKUU 4,516 WAPATIWA MAFUNZO

ADEM kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia chini ya mradi wa BOOST katika kutekeleza Afua namba 8 inayohusu Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa shule na Utawala Bora wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa inaendesha mafunzo kwa Timu za Wawezeshaji (TOT) 255 kwa muda wa siku 3  kuanzia Septemba 21-23, 2023.

 

Mafunzo hayo yanayofanyika ADEM Bagamoyo yamelenga kuwajengea uwezo Wawezeshaji hao watakaofanya uwezeshaji wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Shule na Utawala Bora wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yatakayofanyika kwa Walimu Wakuu 4,516 katika Mikoa 7 ya Tanzania Bara yakilenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji Wasimamizi wa Elimu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. 

 

Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Uendeshaji wa Shule na Utawala Bora wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Walimu Wakuu 4,516 yatafanyika kuanzia tarehe 26 Septamba, 2023.