ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

VIONGOZI 13 WA IDARA YA ELIMU KUTOKA SMZ WANOLEWA ADEM

26 Aug, 2022
VIONGOZI 13 WA IDARA YA ELIMU KUTOKA SMZ WANOLEWA ADEM

Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Siston Masanja Mgullah leo tarehe 25 Agosti, 2022, amefungua mafunzo ya muda mfupi ya siku tano ya Uongozi na Usimamizi wa Skuli pamoja na Uandaaji wa mipango mikakati ya elimu yanayotolewa kwa Viongozi 13 wa elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

 

Mafunzo hayo yameandaliwa na Wakala ambapo wawezeshaji kutoka timu ya Wakala watawajengea umahiri Viongozi hao katika nyanja za uongozi na usimamizi wa elimu.

 

Mafunzo hayo yameanza tarehe 25 Agosti na  yanatarajiwa kumalizika tarehe 29 Agosti, 2022.