ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

MAADHIMISHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, WATUMISHI ADEM WAPIGWA MSASA

04 Jul, 2022
MAADHIMISHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, WATUMISHI ADEM WAPIGWA MSASA

Katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma, ADEM imeendesha Mafunzo Maalum ya Uandaaji mpango wa namna ya kuendelea kutoa huduma wakati na kukabiliana na majanga, wakati Taasisi inapoingia katika changamoto za hatari au migogoro. 

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa siku tatu, kuanzia Juni 22-24 ADEM Bagamoyo na baadae mafunzo hayo yataendeshwa kwa watumishi katika Kampasi za Mbeya na Mwanza.
Mafunzo ya uandaaji wa mpango wa biashara wa kukabiliana na majanga (Business Continuity Plan) yamelenga kuwajengea uwezo watumishi wa Wakala juu ya namna ya kukabiliana na majanga yanapotokea bila kuathiri utoaji huduma za Wakala kwa wateja nawadau wanaohitaji ama kutumia huduma za Wakala.
Akifunga mafunzo hayo Mtendaji Mkuu, Dkt. Siston Masanja Mgullah amewaasa watumishi waliopatiwa mafunzo hayo kuhakikisha kuwa mafunzo waliyopatiwa yamewaongezea ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao na kubadili mtazamo wa namna ya kutenda kisekta ili kufikia malengo ya utoaji huduma bora za Wakala katika nyakati zote hata za majanga.