MAAADHIMISHO YA SIKU YA USHAIRI YAFANA

SIKU YA USHAIRI DUNIANI:
Dar es Salaam
Tarehe 21 Machi, 2025
Karika kuadhimisha siku ya ushairi duniani, Jukwaa la Kiswahili Tanzania limefanya kongamano lilohusisha utoaji wa kuhusu Ushairi na Masuala ya Demokrasia na Siasa Tanzania, Ushairi na Maendeleo ya Tehama Nchini na fani ya Ushairi na mjadala wa kada ya utunzi wake katika karne ya 21.
Kongamano hilo limefanyika leo tarehe 21 Machi, 2025 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Bodi ya Maktaba ambapo Mtendaji Mkuu amewasilisha ya kuhusu Ushairi na Masuala ya Demokrasia na Siasa Tanzania.
Jukwaa la Kiswahili Tanzania ni mtandao wenye lengo la kukuza, kuendeleza na kueneza lugha ya Kiswahili kwa kutumia matamasha, makongamano ya lugha ya Kiswahili, ushairi marathon na ufundishaji wa lugha ya kiswahili kwa wageni.