ADEM Logo

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu

KATIBU MKUU WyEST ASISITIZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA ADEM

22 Dec, 2022
KATIBU MKUU WyEST ASISITIZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI WA ADEM

Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael leo Disemba 22, 2022 amefanya ametembelea Ofisi za Wakala na kuzungumza na watumishi pamoja na wanafunzi wanaoendelea na masomo yao ya Stashahada za Uongozi, Usimamizi na Uthibiti Ubora wa Elimu katika kampasi ya Bagamoyo.Akizungumza katika ziara hiyo Dkt. Francis amesema lengo la kutembelea Wakala ni kuona utekelezaji wa shughuli zinazotekelezwa na Wakala huku akitumia fursa hiyo kusisitiza bidii kwa wafanyakazi.Kwa upande mwingine Dkt. Francis amewaasa wanafunzi wanaosoma masomo ya Uongozi ADEM kuwa, pale watakapohitimu masomo yao na kupata nafasi za Uongozi katika shule wanazosimamia wakahakikishe wanakuwa viongozi na wasimamizi mahiri wa masuala ya elimu na rasilimali za shule kwani Usimamizi ni kuhakikisha vitu vinakwenda na Uongozi unaleta tija na ufanisi katika masuala yote ya Elimu kwani kwa kufanya hivyo wataacha alama ya ufanisi katika uongozi wao.