ADEM NA CHUO CHA TAKWIMU WAKUBALIANA KUSHIRIKIANA ILI KUIMARISHA UTOAJI WA TAKWIMU KATIKA SEKTA YA ELIMU NCHINI

Dar es Salaam: Februari 28, 2025
HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATI YA ADEM NA CHUO CHA TAKWIMU-ESTC
Hafla hiyo imefanyika leo katika Chuo cha Takwimu Changanyikeni Dar Es Salaam ambapo Mtendaji Mkuu - ADEM Dkt. Maulid J. Maulid na Mkuu wa Chuo cha Takwimu Dkt. Tumaini Katunzi wametia saini Mkataba huo unaolenga kuimarisha usimamizi wa takwimu za elimu nchini.
Aidha ushirikiano kati ya ADEM na EASTC utahusisha kubadilishana uzoefu kuhusu usimamizi wa takwimu za elimu, kujengeana uwezo kuhusu usimamizi wa takwimu za elimu, kushirikiana katika kuandika miradi ya kimkakati ya usimamizi wa takwimu na kuisaidia Serikali katika mipango mbalimbali ya elimu na Takwimu hususani Wizara ya Fedha, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja OR-TAMISEMI
@urtmof
@wizara_elimutanzania
@ortamisemi
@chuo_cha_takwimu
@maulidmaulid