ADEM KUENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI, USIMAMIZI NA UTAWALA BORA WA ELIMU KWA MAMENEJA NA WALIMU WAKUU WA SHULE ZA MSINGI NCHINI
13 Jan, 2025

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ameelekeza kutolewa kwa Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi fanisi wa Shule kwa Walimu wakuu na Mameneja wa Shule zisizo za Serikali. Hivyo mafunzo haya yatafanyika kuanzia tarehe 20-22 Januari, 2024 kwa kuanza katika Mikoa ya Arusha, Dodoma na Dar Es Salaam. Ada ya kushiriki mafunzo haya ni Shilingi 970,000/= kwa mshiriki mmoja itakayogharamia i) gharama za ufundishaji, ii) Cheti cha Mshiriki wa mafunzo, iii) Chakula - Chai ya asubuhi, Chakula cha mchana na Chai hya jioni, iv) vifaa vya mafunzo na v) kitabu kuhusu Uongozi, usimamizi na Utawala Bora wa elimu. Ili kujisajili kwa ajili ya kushiriki mafunzo haya tafadhali fuata maelekezo yafuatayo. Mwisho wa kujisajili ni tarehe 18 Februari, 2025